Lugha: Kwa Wakati wa Sasa?
bundle of 10
David Boyd Long
bundle of 10
Ni sharti kwa maneno yote Mkristo anayofanya au kusikia rohoni kupatana na maneno Biblia inayofundisha. Sharti tupime maneno yote na Maandiko Matakatifu. Soma 1 Yoane 2:3-5.Ndani ya Yoane 9 tunasoma habari za mtu
aliyezaliwa kipofu. Mtu huyu alipasha watu
wengine habari za maneno ambayo yalimpata.
Alisema: “Ninajua neno moja, mimi nilikuwa
kipofu, na sasa ninaona” (sh.25).
Maneno yaliyopata mtu huyu yalipatana na
mafundisho ya Biblia. Wafarisayo walitaka aseme
Yesu ni mwenye zambi kama watu wote wengine,
lakini aliwajibu na kusema mwenye zambi hawezi
kufungua macho ya vipofu kwa sababu Mungu
hasikii wenye zambi (sh.31; Zaburi 66:18). Hivi
ajabu hili lilihakikisha ya kwamba Yesu hakuwa
mwenye zambi kama Wafarisayo walivyofikili.
Mtu aliyefunguliwa macho alisema vilevile ya
kwamba Mungu anasikia mtu yule anayefanya
mapenzi yake, na ya kwamba tangu mwanzo wa
dunia halikusikiwa ya kama mtu alifungua macho
ya mwenye kuzaliwa kipofu (mash.31-32). Basi
kama Yesu angalikuwa mtu tu na hakutoka kwa
Mungu, asingaliweza kufanya hivi vile, lakini
alikuwa amefungua macho yake kweli!
Hivi maneno yaliyopata mtu huyu yalipatana
na mafundisho ya Maandiko Matakatifu.
Inatupasa sisi Wakristo kupiga vita vizuri siku
zote na kumaliza mwendo wetu. Pamoja na kufanya
hivi inatupasa kulinda imani, maana yake
kutii Neno la Mungu (2 Timoteo 4:7). Soma 2 Timoteo 2:5 vilevile. Shairi hili linatufundisha ya
kwamba “mtu akishindana katika michezo,
hapewi taji kama asiposhindana kwa halali.”
1 Watesalonika 5:21 linatuagiza kujaribu mambo yote (na Neno la Mungu) na kushika lililo
jema. Haya ni maonyo mazuri, kwani tukitegemea
tu maneno tunayosikia rohoni, ni nyepesi sana
kwa sisi kuanguka. Hivi tujaribu kwa njia ya
Kitabu cha Mungu maneno yote tunayofanya au
kusikia rohoni, na tushikamane na maneno yale tu
yanayopatana na mafundisho ya Biblia.
David Boyd Long
David Boyd Long was born in Ireland and served as a missionary in Angola for over 30 years. The primary focus of his ministry was translating the Bible into Chokwe and teaching the Word over a wide area. When the Longs had to leave Angola because of the civil war, they returned to Canada, continuing a widely accepted ministry around the world. Mrs Long passed away in 1982; Mr Long remarried the following year; subsequently moving back to Ireland where he passed away early in 2007.












