Mafundisho juu ya Biblia AGANO JIPYA: Matayo - Matendo

William MacDonald

$4.39

Maelezo ya Maandiko Matakatifu kwa Waamini

UTANGULIZI WA MWANDISHI

Kusudi la Kitabu hiki cha Mafu ndisho juu ya Biblia kwa Waamini ni kusaidia Mkristo kujifunza Biblia na kuendelea kujuana na Maandiko Matakatifu. Lakini hakuna kitabu cha Mafundisho kinachoweza kukomboa faida ya Biblia yenyewe. Kinaweza kueleza tu maana yake na kusaidia msomaji kufahamu maneno anayosoma yeye mwe nyewe ndani ya Maandiko Matakatifu. Ninaamini kabisa ya kwamba Mkristo ye yote anayedumu kusoma na kujifunza Neno la Mungu anaweza kugeuka �mfanya kazi asiyeona haya, akifasiri vema neno la kweli� (2 Tim. 2:15).

Lakini kujua tu maneno ya Biblia hakutoshi. Ni lazima kwa msomaji kutii mafundisho yake ndani ya maisha yake ya kila siku. Kwa sababu hii mwandishi wa kitabu hiki cha Mafundisho anajaribu sana kuonyesha namna gani msomaji anaweza kuwa mtendaji wa Neno la Mungu, si msikiaji tu.

Msomaji akisoma kitabu hiki cha Mafundisho peke yake, pasipo Biblia, kitabu hiki hakitamsaidia, lakini kitageuka mtego kwake. Kitakuwa na faida tu kama kikiongeza hamu yake kutafuta Maandiko yeye mwenyewe na kutii maagizo ya Bwana.

Ninaomba Roho Mtakatifu, aliyeongoza kuandika kwa Biblia, afungue na kutia nuru nia ya msomaji wakati anapojitoa kwa neno hili zuri zaidi � kujua Mungu kwa njia ya Neno lake.

William MacDonald

William MacDonald (January 7, 1917 - December 25, 2007) has authored over eighty books dealing with subjects such as evangelism and discipleship, church life, marital relations, as well as a best-selling Bible commentary. While pursuing a degree at Harvard (MBA), the Lord called him into the ministry. He served as President of Emmaus Bible College, as well as teaching many classes. He and O. Jean Gibson founded a discipleship school for young men at Fairhaven Bible Chapel in northern California. A favorite Bible teacher to many, he traveled and spoke at conferences throughout the United States and Canada. He makes his home in Heaven.

Related Products

More Titles by William MacDonald

Newsletter Sign Up