Tukitazama Yesu

Theodore Monod

$2.50

Maneno mawili tu, lakini ndani ya maneno haya mawili inafichwa siri nzima ya maisha ya baraka.

TUKITAZAMA YESU, katika Maandiko Matakatifu, kujifunza pale kama alikuwa nani, kazi aliyofanya, vitu anavyotoa, na vitu anavyotaka; kuona ndani yake mfano wa kuiga, kujifunza kwa njia ya mafundisho yake, kuona ndani ya maagizo yake sheria yetu, kutegemea ahadi zake, kuona ya kama Yeye Mwenyewe na kazi zake zinaweza kushibisha kila hitaji la roho zetu.

TUKITAZAMA YESU, aliyetukuzwa, kuona ya kwamba Yeye ndiye Mwombezi wetu mbinguni, anayetimiza kwa njia ya kutuombea kazi iliyohitajiwa kwa wokovu wetu, kazi ambayo mapendo yake makubwa yalimsukuma kufanya (1 Yoane 2:1); Yeye anayefika mbele ya Mungu hata sasa kwa ajili yetu (Ebr. 9:24), Kuhani la kifalme, sadaka bila kipaku, akichukua daima uovu wa vitu vyetu vitakatifu (Kutoka 28:38).

Related Products

Newsletter Sign Up