Series: Visa Vya Biblia

Visa Vya Biblia: Sehemu ya Pili

Marian Schooland

$10.25

Habari waziwazi za Agano Jipya pamoja na mifano

Zamani sana sana, Mungu alitoa ahadi. Alisema atatuma Mfalme mkubwa kwa watu wake. Mfalme huyu atakuwa Mfalme mkubwa sana. Atakuwa mkubwa kuliko wafalme wote wengine walioishi mbele. Hakuna mfalme mwingine atakayeweza kuwa mkubwa kama Yeye. Atafanya maajabu mengi.

Ataponyesha macho ya vipofu waweze kuona tena. Atafungua masikio ya viziwi. Ataponyesha wagonjwa. Ataokoa watu wake toka zambi zao.

Kwa wakati ule watu wa Mungu walikuwa Wayuda. Walikaa katika Palestina. Walikuwa na mji mkubwa ulioitwa Yerusalema. Na ndani ya Yerusalema kulikuwa Hekalu zuri sana.

Hekalu hili lilikuwa nyumba ya Mungu ya Wayuda. Walikwenda Hekaluni kila siku kuabudu Mungu.

Wayuda walifurahi sana juu ya ahadi ya Mungu. Walifurahi kufikili ya kwamba watakuwa na Mfalme mkubwa wa namna hii siku nyingine.

Miaka mingi ilipita. Yule Mfalme mkubwa hakufika. Watu walingoja sana kwa Mungu kumtuma. Ni kama iliwapasa kungoja miaka mingi sana.

Lakini Mungu anatimiza ahadi zake kila mara. Naye anatengeneza maneno yote vizuri. Anafanyiza maneno kutokea kwa saa nzuri.

Basi kwa mwisho siku ya kuja kwa Mfalme mkubwa ilifika.

Halafu Mungu alituma malaika - malaika ya kungaa toka mbinguni. Akatuma malaika huyu duniani kutayarisha maneno kwa kuja kwa Mfalme mkubwa.

This book is a Bible story book for children with stories from the New Testament.

Related Products

More Titles by Marian Schooland

Newsletter Sign Up