Series: Visa Vya Biblia

Visa Vya Biblia: Sehemu ya Kwanza

Marian Schooland

$12.50

Habari waziwazi za Agano la Kale pamoja na mifano

Zamani sana watu hawakuwa, hata mmoja. Hata ulimwengu haukuwa. Jua halikuwa mbinguni; mwezi wala nyota hazikuwa. Katika nafasi kubwa zote kitu hakikuwa hata kimoja. Mungu tu alikuwa, na Mungu alikuwa pahali po pote. Lakini Mungu alikuwa na shauri katika nia yake. Alisema: «Tutafanya watu. Na tutafanya dunia nzuri waweze kukaa ndani yake. Tutafanya jua na mwezi na nyota nyingi ziwatolee nuru zao.»

Hivi Mungu alifanya kitu kilichoonekana kama mpira mkubwa sana mviringo. Tunaita mpira ule dunia au ulimwengu. Sisi tunakaa juu ya mpira mkubwa ule ndiyo dunia. Kwa mwanzo dunia ilikuwa giza kama katikati ya usiku. Na ilifunikwa na maji. Lakini Roho ya Mungu alikuwa pale katika giza na maji yale. Halafu Mungu alisema: «Nuru iwe.» Na nuru ilikuwa. Nuru iliangaza dunia. Ile ilikuwa asubui ya kwanza; asubui ya siku ya kwanza.

Siku ya kwanza ilipita na nuru ilikwisha. Usiku uliingia; na dunia nzima ilikuwa giza tena. Lakini asubui ilifika tena — asubui ya pili. Nuru iliangaza dunia tena.

Asubui ya pili Mungu alitoa agizo kwa maji. Wakati Mungu alipotoa agizo, nusu ya maji yalikwenda mbinguni na yaligeuka kuwa mawingu. Nusu yake yalibaki chini duniani. Hivi maji yalikuwa mbinguni, ndani ya mawingu, na maji yalikuwa pahali po pote duniani.

This book is a Bible story book for childrn with stories from the Old Testamtent.

Related Products

More Titles by Marian Schooland

Newsletter Sign Up