Kusanyiko la Wakristo-Kanisa ni Nini?

Robert Cullen M.N. Wolcott

$2.50

“lakini takaseni Kristo kuwa Bwana mioyoni mwenu, mukiwa tayari wakati wote kujibu kila mtu anayeuliza habari za tumaini lililo ndani yenu; lakini kwa upole na kuogopa” (1 Petro 3:15).

NENO TOKA MTAFSIRI

Kitabu hiki kidogo kiliandikwa kwanza na lugha ya kiengereza na Robert Cullen, aliye mtumishi wa Bwana Yesu Kristo kwa inchi ya Uganda. Rafiki zake za Uganda wanamjua kwa jina la “Bob”. Bob anafundisha Biblia na watu wanaofurahi kukutana naye mara na mara. Kitabu hiki kilizaliwa kwa majifunzo yale.

Niliwaza ya kuwa mafundisho haya juu ya Kanisa yanahitajiwa sana katika lugha ya kiswahili. Kwa wakati wetu wa sasa zaidi ya watu wanafuata desturi za makanisa bila kutafuta mafundisho wazi ya Agano Jipya. Kumbe desturi za watu mara nyingi ni uadui wa wale wanaotaka sana kufuata Maandiko Matakatifu.

Bwana wetu alisema “nitajenga kanisa langu...” (Matayo 16:18). Na sisi, watumwa wanyenyekevu wasio na faida tunaofanya tu maneno ambayo inatupasa kufanya, tunaitwa kutumika pamoja naye katika kazi takatifu ya kujenga makanisa kwa utukufu wake. Mtume Paulo alisema ya kwamba alijenga kwa mji wa Korinto, akiweka msingi wa kanisa pale (soma 1 Wakorinto 3:10-15). Wengine waliendelea kujenga nyuma yake. Na sasa sisi watumishi wa wakati wa sasa, tunajenga makanisa pamoja na Bwana wetu. Paulo anatushauri kuangalia sana kwa namna tunavyojenga makanisa, kwa sababu kazi yetu itafunuliwa wazi na itajaribiwa na moto. Kwanza tuhakikishe ya kwamba tunajenga juu ya msingi wa Yesu Kristo mwenyewe. Tena tuchague vitu vya kudumu kujenga navyo, kama zahabu na feza na mawe ya bei kubwa.

Mungu atuletee uhodari kuachana na desturi za watu zilizo kama miti na nyasi zenye kuungua mbio kwa moto wa kujaribiwa wa Mungu, na kutafuta kusimamisha makanisa ya Bwana Yesu kwa sura ya makanisa ya Agano Jipya. Tutaheshimu Bwana wetu na tutafungua njia ya kumtukuza sana kama tukifuata mafundisho ya Neno lake. Tutafute sana uongozi wa Roho Mtakatifu kutuonyesha kutaka kwa Bwana kwa Kanisa lake, ambalo alinunua na bei ya damani ya damu yake mwenyewe. Tukifahamu kutaka kwake kwa Kanisa lake, tusiwe wenye kusikia tu, lakini wenye kutii Neno lake na wenye kutenda kupatana na elimu tunayofahamu. M. N. Wolcott, mtafsiri

Related Products

More Titles by M.N. Wolcott

Newsletter Sign Up