Translations

Pictures Of ChristFiguras de Cristo

Mifano ya Kristo

William A. Deans

$4.50

Katika Agano la Kale

TANGAZO

Biblia ni maandiko ambayo Mungu aliletea watu. Ina vitabu 66 ndani yake, vilivyo katika sehemu kubwa mbili. Sehemu hizi, ndizo Agano la Kale na Agano Jipya, zinafungana kuwa moja. Sehemu moja ya Biblia inatusaidia kufahamu sehemu ya pili.

Agano la Kale liliandikwa zamani sana, mbele ya kuzaliwa kwa Bwana Yesu Kristo. Watu watakatifu waliongozwa na Roho Mtakatifu kuandika maneno Mungu aliyotaka kujulisha watu.

Hata Agano la Kale liliandikwa mbele sana ya kuzaliwa kwa Bwana Yesu, lina mifano mingi juu yake inayofanana naye katika maisha yake, mauti yake, ufufuko wake, utumishi wake wa sasa na utakatifu wake wa nyuma.

Kuna unabii kupasha habari za mambo yatakayotukia nyuma, kutabiri vitu visivyotukia bado. Agano la Kale lina unabii juu ya Kristo na vilevile mifano mingi ya ajabu juu yake. Mifano hii inaonekana ndani ya maisha ya watu wa zamani, na katika mambo yaliyotukia juu ya Waisraeli. Vilevile katika mambo ya hema ya kusanyiko jangwani kuna maana nyingi za faida sana kueleza uzuri wa Kristo na utumishi wake.

Mara nyingine matukio haya ya nyakati za zamani yanaonyesha mifano ya Kristo waziwazi. Mara nyingine yanaonekana kama vivuli kuonekana nusu nusu. Ni kama kivuli cha mtu kinachoonekana mbele ya kufika kwake mwenyewe, kueleza namna yake kwa sehemu tu, si wazi sana.

Kwa kuyafahamu kabisa tunahitaji kusoma Agano Jipya. Pale mara nyingi maelezo ya mifano yanaonekana wazi kutufunulia maana zao kabisa. Hivi tutatafuta mfano wa Kristo katika Agano la Kale, halafu tutapeleleza katika Agano Jipya kupata mashairi kueleza maana yake.

Tutatumika na Biblia nzima pamoja na kitabu hiki kwa kufahamu haki ya Mwokozi Yesu. Tuombe Mungu atuonyeshe Kristo katika mifano hii. Tutashangaa na raha kwa kuona namna Agano la Kale linavyofungana pamoja na Agano Jipya kutufunulia uzuri wa Kristo na damani ya matendo yake.

Kama ukipenda Bwana Yesu na moyo wako, na ukiamini Neno lake kabisa, utapata furaha kwa kusoma maelezo ya kitabu hiki. Utajifunza maneno mengine mengi juu ya Mwokozi wako ambaye unapenda.

Soma mashairi haya katika Biblia yako. Pale utafahamu Maandiko Matakatifu yalitolewa na Mungu kwa njia ya mitume yake. Hata manabii ya zamani walitabiri juu ya Yesu. Soma mashairi haya : 2 Timoteo 3:16; 2 Petro 1:20-21; Yoane 8:56; Yoane 5:39,46; Zaburi 40:7; Waebrania 10:7; Matayo 22:45

William A. Deans

William Alexander Deans (1908-1999) served the Lord as a missionary in northeast Belgian Congo (now the Democratic Republic of Congo) He was active in the publishing of Christian literature in African languages including the Babira, Pygmy, Wabira, Wahema, Wangeti, and Walesi tribes.

Related Products

More Titles by William A. Deans

Newsletter Sign Up