Translations

Mark & the Untiring Servant

Habari Njema ya Marko

Jean Dougan

$5.75

Habari Njema Yoane Marko aliyoandika ni fupi kupita Habari Njema ya Matayo, Luka au Yoane, lakini hata hivi aliandika juu ya maneno mengine ambayo wale waandishi watatu wengine hawakuandika juu yao.

  • SKU: 131
  • ISBN: 978-0-88873-131-9
  • Page Count: 88
  • Language: Congo Swahili
  • Format: Paperback
  • Binding: Perfect Binding
  • Category: Bible Study
  • Topics:  Mark

HABARI NJEMA YA MARKO
Utangulizi

Habari Njema Yoane Marko aliyoandika ni fupi kupita Habari Njema ya Matayo, Luka au Yoane, lakini hata hivi aliandika juu ya maneno mengine ambayo wale waandishi watatu wengine hawakuandika juu yao. Marko alikuwa mwanafunzi wa Bwana, lakini hakuwa mmoja wa mitume kumi na wawili (Marko 3:16-19). Mama yake alikuwa ameamini Kristo na alitumia nyumba yake kwa kazi ya Bwana (Matendo 12:12). Marko alikuwa mjomba wa Barnaba (Wakolosayi 4:10).

Kwa Matendo 11:29-30 tunasoma ya kwamba ndugu za kanisa kwa Antiokia walituma Barnaba na Paulo kwa Yerusalema na zawadi zao kusaidia waamini wa pale, na Marko alikwenda pamoja nao wakati waliporudia Antiokia (Matendo 12:25). Kwa Matendo 13:2 tunasoma ya kwamba Roho Mtakatifu aliagiza wazee wa kanisa kwa Antiokia kutuma Baraba na Paulo kuhubiri Habari Njema. Walipeleka Yoane Marko pamoja nao kuwasaidia (Matendo 13:5). Lakini kwa shairi 13 tunasoma ya kwamba Yoane Marko aliwaacha wakati walipofikia Perga, akarudia Yerusalema.

Paulo hakupendezwa hata kidogo juu ya neno hili na nyuma alikataa kupeleka Marko pamoja nao kwa safari nyingine ya kuhubiri hata kama Barnaba alitaka aende pamoja nao (Matendo 15:37-39). Marko alikuwa amewaacha mbele na Paulo hakuwa tayari kumwamini tena. Alibishana na Barnaba juu ya neno hili bila kupatana, basi wali- achana. Halafu Paulo alichagua Sila kwenda pamoja naye kwa pahali pa Marko na Barnaba na Marko walikwenda pamoja. Ni kama kanisa walikubali neno Paulo alilofanya kwani kwa shairi 40 waliomba bara- ka ya Mungu juu ya Paulo na Sila mbele ya kuondoka kwao. Hatusomi juu ya Marko tena ndani ya kitabu cha Matendo.

Ni vizuri kuona ya kwamba hata hivi Marko aligeuka mtumishi wa faida wa Bwana Yesu. Paulo alisema nyuma ya kwamba alifarijiwa na Marko (Wakolosayi 4:10-11), na kwa 2 Timoteo 4:11 alisema na Timoteo kutwaa Marko na kumleta pamoja naye kwa sababu “ananifaa kwa utumishi.” Tutaona ya kwamba ndani ya Habari Njema yake Marko alionyesha Bwana Yesu kama Mtumishi MKAMILIFU.
Tunaweza kugawa kitabu hiki kwa sehemu tatu:
1. Mwanzo 1:1-13
2. Utumishi bila kuchoka 1:14 – 10:52
3. Kutii hata mauti 11:1 – 16:20

Habari Njema ine zinatuonyesha Bwana Yesu kwa njia mbalimbali. Matayo anamwonyesha kama Mfalme, Marko kama Mtumishi, Luka kama Mwana wa watu na Yoane kama Mwana wa Mungu. Matayo alianza kitabu chake kwa njia ya kuita Yesu “Mwana wa Daudi,” mfalme. Halafu alitaja majina ya wazazi wake hapa duniani kuanza na Abrahamu. Nyuma ya mashairi machache ya kuanza nayo Luka ali- pasha habari za kuzaliwa kwa Yoane Mbatizaji, kisha habari za kuzali- wa kwa Bwana Yesu (Mwana wa watu). Yoane alianza Habari Njema yake kwa njia ya kusema mara moja juu ya Yesu Kristo, Mwana wa milele wa Mungu, “Katika mwanzo alikuwa Neno (Yesu Kristo) na Neno alikuwa pamoja na Mungu, na Neno alikuwa Mungu” (Yoane 1:1).

Jean Dougan

Canadian author Jean Dougan (1916-2003), was a home maker, poet, and author. For years she has written poems for Smoke Signals a camp magazine; and every year the words for the camp hymn. These hymns have been published under the title Themes from the Classics. Mrs. Dougan has also contributed to five volumes of The Looking Glass, daily devotional readings for teens. Jean Dougan has drawn many practical lessons from the Living Word of God.

Related Products

More Titles by Jean Dougan

Newsletter Sign Up