Translations

The Church of the New TestamentA Igreja do Novo Testamento

Kanisa la Agano Jipya

R. E. Harlow

$4.50

Ndani ya Biblia, Neno takatifu la Mungu. Biblia iliandikwa kwa maongozi ya Roho Mtakatifu nayo peke yake ina amri kutufundisha namna gani tunaweza kuanza kanisa ao kuliongoza. Na Biblia inatosha kabisa kutuonyeshea mapenzi ya Mungu kwa maneno haya.

PAHALI GANI TUNAWEZA KUJIFUNZA JUU YA KANISA?

Ndani ya Biblia, Neno takatifu la Mungu. Biblia iliandikwa kwa maongozi ya Roho Mtakatifu nayo peke yake ina amri kutu- fundisha namna gani tunaweza kuanza kanisa au kuliongoza. Na Biblia inatosha kabisa kutuonyeshea mapenzi ya Mungu kwa maneno haya.

Kwa wakati wa mwanzo Mungu aliumba nyama wote, kisha aliumba mtu wa kwanza, ndiye Adamu. Mtu ni namna nyingine na nyama kwani ana roho na anaweza kusikia sauti ya Bwana ikisema naye. Na Mungu ana amri kutuambia maneno anayota- ka sisi kufanya.

Zamani Mungu alisema mara nyingi kwa manabii wake waaminifu, na nyuma alisema katika Mwana wake, Bwana Yesu Kristo (Waebrania 1:1,2). Kristo alikufa na alifufuka tena na ali- tuma Roho Mtakatifu kukaa ndani ya mioyo yetu. Roho Mtakatifu alisema kwa njia ya mitume na waandishi wengine wa Agano Jipya (Yoane 14:26; 16:13,14).

Mitume walijua ya kwamba walikuwa wakiandika maneno ambayo Mungu aliwaagiza kuandika. Paulo alisema ya kwamba alipokea toka Bwana kweli ya Habari Njema (1 Wakorinto 15:3), na aliihubiri kwa watu. Hili ndilo neno kubwa, na Roho Mtakatifu aliongoza Paulo kuongeza ya kwamba mtu ye yote anayefundisha “habari njema” nyingine atalaaniwa na Mungu (Wagalatia 1:8,9,12,16).

Paulo alifundisha “kwa neno la Bwana” ya kwamba Kristo atakuja tena kupeleka Kanisa lake kwake (1 Watesalonika 4:15).

Alipokea ufunuo toka Bwana juu ya Meza ya Bwana, ndiyo Karamu ya Ukumbusho wa kufa kwa Kristo (1 Wakorinto 11:23). Bwana alimfunulia vilevile kweli ya umoja wa Kanisa (Waefeso 2:3,6). Tutajifunza zaidi juu ya maneno haya nyuma kidogo ndani ya kitabu hiki, lakini hapa tuone tu ya kwamba Paulo ali- jua alikuwa akisema na kufundisha maneno ambayo Mungu alimfundisha yeye.

Paulo alijua ya kwamba aliandika maagizo ya Bwana na ya kwamba Roho Mtakatifu alisema naye (1 Wakorinto 14:37; 1 Timoteo 4:1). Ndiyo, alisema maneno yale yale ambavyo Roho Mtakatifu alimwongoza kusema (1 Wakorinto 2:10,12,13).

Petro alipatana na Paulo ndani ya maneno haya. Petro na mitume yote waliamini kabisa ya kwamba Agano la Kale ni Neno la Mungu, lakini tunajua alihesabu maandiko ya Paulo kuwa kipimo kimoja na maandiko ya Agano la Kale kwa sababu aliyaita “Maandiko” vilevile (2 Petro 1:21; 3:16). Ndiyo, alihesabu masemo ya mitume na hata maandiko yake mwenyewe kuwa kipimo kimoja na masemo ya manabii watakatifu wa zamani (2 Petro 3:2). Petro alisema ya kwamba tunazaliwa tena kwa Neno la Mungu, na ya kwamba tunapata nguvu katika imani kwa njia ya Neno la Mungu vilevile (1 Petro 1:23; 2:2).

Mtume Yoane aliandika maneno yote ambayo Bwana ali- mfunulia (Ufunuo 1:2,19; 2:1,8,12,18; 3:1,7,14; 4:1; 6:1; 14:13; 19:9; 21:5).

Paulo alisema ya kwamba kila andiko (ndiyo Maandiko Matakatifu) limepewa kwa maongozi ya Mungu, na linafaa kwa mafundisho (2 Timoteo 3:16), na alitaja Agano la Kale pamoja na Agano Jipya (1 Timoteo 5:18). Tunajua kabisa ya kwamba Agano Jipya ni Neno la Mungu na ya kwamba linatufundisha namna gani Mungu anataka sisi kujenga kanisa.

R. E. Harlow

Robert E. Harlow,a long-time commended worker, went to be with the Lord on March 10, 2003, five days short of his 95th birthday. He was co-founder of Emmaus Bible College, now located in Dubuque, Iowa, and founder, along with his wife, Gertrud, of Everyday Publications, Inc., in Port Colborne, ON. Dr. Harlow wrote more than fifty books, including Come and Dine: New Testament Readings for Every Day (1976). His,Can We Know God? (1958) was the first of a series of books he wrote in simple, "Everyday", English. It has sold some 500,000 copies in more than a dozen languages. A native of Toronto, he was also a missionary in the Belgian Congo.

Related Products

More Titles by R. E. Harlow

Newsletter Sign Up