Translations

Matthew: Presenting - Jesus The KingMateo: Presentando a Jesús el Rey

Habari Njema ya Matayo Juu ya: Yesu Mfalme

Robert Henry Sykes

$11.75

Matthew

  • SKU: 121
  • ISBN: 978-0-88873-121-0
  • Page Count: 210
  • Language: Congo Swahili
  • Format: Paperback
  • Binding: Perfect Binding
  • Category: Bible Study
  • Topics:  Matthew

Kitabu cha Matayo ni kitabu cha kwanza ndani ya Agano Jipya. Ni ka-ma mlango toka Agano la Kale kuingia Agano Jipya. Ndani ya Agano la Kale manabii walitabiri maneo mengi juu ya Mwokozi na Mfalme ambaye atakayekuja, atakuwa namna gani, maneno gani atakayofanya na nini itampata.

Habari Njema ya Matayo
juu ya
YESU MFALME

Kitabu cha Matayo ni kitabu cha kwanza ndani ya Agano Jipya Ni ka ma mlango toka Agano la Kale kuingia Agano Jipya. Ndani ya Agano la Kale manabii walitabiri maneno mengi juu ya Mwokozi na Mfalme ambaye Mungu aliahidi kutuma. Unabii wao ulionyesha kama Mfalme atakayekuja atakuwa namna gani, maneno gani atakayofanya na nini itampata.
Roho ya Mungu aliongoza Matayo kuonyesha Bwana Yesu Kristo kama Mfalme kwa taifa la Israeli. Hivi Matayo alitaja mashairi mengi toka maandiko ya Agano la Kale, ndilo Biblia ya Waisraeli. Mashairi haya yalikuwa juu ya Masiya atakayekuja na Matayo aliyataja kusaidia Waisraeli (na sisi) kutambua Mfalme huyu mkubwa na kuinama mbele yake kumwabudu na kumtii.
Waandishi wengine wa Agano Jipya walitaja mashairi toka Agano la Kale vilevile, lakini hawakutaja mashairi mengi sana kama Matayo. Matayo alitaja mashairi kupita 250 ya Agano la Kale ndani ya kitabu chake zaidi ya yale juu ya kizazi cha Bwana Yesu. Mashairi haya yanatoka ndani ya kila kitabu cha Agano la Kale ila Mhubiri, Wimbo wa Solomono, Obadia, Nahumu na Habakuki. Hivi Matayo anaonyesha wazi yule aliye Mwokozi na Mfalme ambaye Mungu aliahidi kutuma. (Soma Yoane 10:1-3.) Anahakikisha tena na tena ya kwamba Yesu Kristo ndiye Mfalme kwa njia ya kumsawanisha na maneno yale yaliyoandikwa juu yake ndani ya Agano la Kale. Wakati tutakaposoma kitabu cha Matayo pamoja, labda utataka kuandika mashairi haya toka Agano la Kale kando ya pahali yanapotimizwa ndani ya Matayo.
Ndani ya sura 1 na 2 tutasoma juu ya kizazi na kuzaliwa kwa Mfalme huyu mkubwa.
Ndani ya sura 3 tunasoma juu ya mjumbe na mtangulizi wa Mfalme.
Sura 4-18 zinapasha habari za utumishi wa ufalme katikati ya watu, zaidi katika Galilaya.
Ndani ya sura 19 na 20 Mfalme anasafiri toka Galilaya kwe nda Yerusalema, mji wa Mfalme mkubwa.
Ndani ya sura 21-27 tunamwona katika Yerusalema, Mfalme aliyekataliwa na watu na aliyehukumiwa na kuuawa.
Ndani ya sura 28 anafufuliwa toka wafu na anaonekana kwa wafuata wake.
Itakusaidia kufuata safari za Mfalme juu ya ramani. Kuna ramani nzuri kwa mwisho wa Biblia yako? Wakati unaposoma kitabu cha Matayo tafuta kila pahali Bwana Yesu alipofikia na andika mistari toka pahali pamoja hata pahali pa kufuata. Utaona ya kwamba kufika sura 21 alishinda zaidi katika Galilaya. Tutaona nyuma sababu kwa neno hili.

Robert Henry Sykes

Robert Henry Sykes was born in Michigan and served in the business world for many years. He and his wife, Wilma, were commissioned by their home church in Grand Rapids for missionary work in Angola. Now living in Montana, Bob Sykes is busy in a Bible teaching and church planting ministry.

Related Products

More Titles by Robert Henry Sykes

Newsletter Sign Up