Omba kwa Jina Langu - 171

$title Anwani: Omba kwa Jina Langu
Mwandishi: Gertrud Harlow
Format: Paperback
Jalada: Saddle-Stitch Binding
Ukubwa wa kitabu: 5.5x8.5x0.10
Aina: Doctrinal Books
Jambo la kufikiriwa: Prayer
Hesabu ya kurasa: 32
Mtoa Vitabu: Everyday Publications Inc.
ISBN-13: 978-0-88873-171-5
Bei: $2.25 (CDN)
Lugha nyingine: Everyday English, Spanish & French


Kusoma…

"Na mukiomba lo lote kwa jina langu, nitalifanya, Baba atukuzwe ndani ya Mwana. Kama mukiomba neno gani kwa jina langu nitalifanya." [Yoane 14:13-14]

          Nani alisema maneno haya matamu katika Yoane 14:13-14? Bwana Yesu Kristo, Mwana wa Mungu. Alikuwa akifundisha wanafunzi juu ya maombi, na pamoja na agizo hili kuomba kwa jina lake aliwapa ahadi ya ajabu: alisema atafanya neno lo lote ambalo wataliomba, ili Mungu Baba atukuzwe ndani ya Mwana wake.

          Maombi ni nini? Ni kuomba Mungu Baba kwa jina la Mwana wake, ndiye Bwana Yesu Kristo, kutupa sisi vitu tunavyohitaji, na kuweka mbele yake maneno mbalimbali mengi tunayotaka afanye kwa sisi na kwa watu wengine.

          Ndani ya masomo utaona, kwa ufupi, zaidi ya maneno ambayo Neno la Mungu linatufundisha juu ya maombi. Roho Mtakatifu tu anaweza kukufundisha kuomba, kama ukimpa njia kufanya hivi. Lakini sharti ujue maneno ambayo Mungu anatufundisha juu ya maombi ndani ya Kitabu chake.

          Kitabu hiki kina sehemu au sura 12. Utasaidiwa zaidi kama ukisoma sehemu moja kila siku ukisoma kila shairi linalotajwa ndani ya Biblia yako mwenyewe.

          Tunaomba Mungu aweze kutumika na kitabu hiki kidogo kuongeza hamu yako kusemezana na kushiriki na Mungu kwa njia ya maombi.
 
Go to the Top