Uongozi Katika Kanisa

Kawaida ya Uongozi Katika Biblia
By Roger Rayhbuck

Uongozi Katika KanisaTitle: Uongozi Katika Kanisa
Author: R. Rayhbuck
Language: Congo Swahili
Format: Paperback
Binding: Perfect Binding
Book Size: 5.5x8.5x0.10
Category: Doctrinal
Topic: The Church
Page Count: 40
Publisher: Everyday Publications Inc.
ISBN-13: 978-0-88873-143-2
Item Code:  143
$ 2.75 
(CDN)

Description

UTANGULIZI

Wakubwa wa Biblia wote walitambua ya kwamba ni lazima watu wa Mungu wawe na waongozi wema. Kwa mfano, Musa alisema na Mungu, “Bwana Mungu... aweke mtu juu ya makutano... ili makutano ya Bwana wasiwe kama kondoo wasio na mchungaji,” (Hes. 27:16,17). Wakati Waisraeli walipokuwa na waongozi wema walibarikiwa na Mungu, lakini wakati walipokuwa na waongozi wabaya waliteseka. Mara tatu Bwana Yesu aliagiza Petro kulinda kondoo zake (Yn. 21:16). Wakati Paulo alipoagana na wazee wa Efeso aliwakumbusha ya kwamba Roho Mtakatifu aliwafanyiza waangalizi kusudi wachunge kanisa la Mungu (Mdo. 20:28). Vivyo hivyo, Petro alisihi wazee wa Asia kulinda kondoo za Mungu (1 Pet. 5:2).

Agano Jipya linatufundisha ya kwamba ni kazi ya wazee kuchunga na kulisha kondoo za Mungu. Lakini nyuma ya muda wa Agano Jipya, kanisa la Mungu lilianza kubadilika. Magawanyiko yalianza kuonekana katikati ya Wakristo na wao walioitwa na Mungu kuwasaidia na kuwachunga. Nyuma kidogo, wazee wa kanisa walikombolewa na makuhani, maaskofu, na watu wengine waliopata pahali pa heshima katika uongozi wa kanisa. Zaidi, uongozi na uchungaji kwa kundi la wazee umepotea katika makanisa.

Leo, katika makanisa mengi, kuna ukosefu wa kufahamu kazi na mamlaka ya wazee. Kusudi la maandiko haya ni kuonyesha kitu gani Biblia inatufundisha juu ya wachungaji wa kanisa. Ninasihi watu wanaosoma maandiko haya kuangalia kila shairi linalotajwa ndani yake, na kuomba Mungu aonyeshe namna gani kuturudisha kwa njia yake ya uongozi (2 Tim. 2:15).

Biography of 

 More…


Other Titles by Roger Rayhbuck


Bible

  Spiritual Growth

   Bible Study

    Doctrinal

    Youth Books

     Devotional Books

      Missionary Books

       Other Books

        Hymn Books