Barua za Agano Jipya

Everyday English   Spanish   

Kitabu hiki kiliandikwa zaida kwa watu wa Afrique.
By Albert E. Horton

Barua za Agano JipyaTitle: Barua za Agano Jipya
Author: A. Horton
Language: Congo Swahili
Format: Paperback
Binding: Perfect Binding
Book Size: 5.5x8.5x0.35
Category: Bible Study
Topic: Romans, 1 Corinthians
Page Count: 144
Publisher: Everyday Publications Inc.
ISBN-13: 978-0-88873-167-8
Item Code:  167
Other Languages: EEES
$ 8.50 
(CDN)

Description

Kitabu hiki kiliandikwa zaidi kwa watu wa Afrique. Mafundisho juu ya kila barua ni mafupi tu na mwandishi alijaribu kuonyesha maneno makubwa makubwa yaliyo katika kila barua. Hakujaribu kueleza maneno yote yote ndani ya kila barua. Tunataraji mafundisho ya kitabu hiki yatasaidia msomaji kufahamu barua za Agano Jipya vizuri zaidi, hata aweze kuzisoma na kujifunza ndani yao yeye mwenyewe na kupata faida nyingi.

Kitabu hiki kiliandikwa zaidi kwa watu wa Afrique. Mafundisho juu ya kila barua ni mafupi tu na mwandishi alijaribu kuonyesha maneno makubwa makubwa yaliyo katika kila barua. Hakujaribu kueleza maneno yote yote ndani ya kila barua. Tunataraji mafundisho ya kitabu hiki yatasaidia msomaji kufahamu barua za Agano Jipya vizuri zaidi, hata aweze kuzisoma na kujifunza ndani yao yeye mwenyewe na kupata faida nyingi.

Vitabu vine vya kwanza katika Agano Jipya vinaitwa Habari Njema. Ndani ya Habari Njema hizi tunasoma habari nzuri juu ya kuja kwa Mwokozi, juu ya kazi yake na maisha yake katikati ya watu, juu ya mauti yake kwa ajili yetu na juu ya ufufuko wake toka wafu.

Kitabu cha tano cha Agano Jipya kinaitwa Matendo ya Mitume. Ni watu waliochagua majina haya kwa vitabu vile vitano vya Agano Jipya. Maneno yaliyoandikwa ndani ya vitabu hivi zamani, yaliandikwa kwa kuongozwa kwa Mungu na hivi makosa hayako ndani yao. Lakini majina ya vitabu vile ha - yakuwekwa kwa kuongozwa kwa Mungu. Labda jina zuri zaidi kwa Matendo ya Mitume ni “Matendo ya Roho Mtakatifu”, au “Mambo Kristo aliyofanya nyuma ya ufufuko wake, akitumika kwa njia ya Roho Mtakatifu”. Kitabu cha Matendo ya Mitume kinatuambia namna gani kanisa lilianzwa, wakati Roho Mtakatifu alipokuja, na namna gani waamini wa kwanza walitumika kwa kupasha watu wengine juu ya ufufuko wa Kristo toka wafu.

Kitabu cha mwisho cha Agano Jipya kinaitwa Ufunuo. Ndani ya Biblia nyingine, tunaona jina hili “Ufunuo wa Yoane”. Lakini jina hili si sawa. Kabisa kabisa ni “Ufunuo wa Yesu Kristo”, kama tunavyoona ndani ya shairi la kwanza la Kitabu hiki. Kitabu cha Ufunuo kinatupasha juu ya utukufu wa Bwana wetu Yesu Kristo sasa kule mbinguni, na juu ya maneno yatakayotokea nyuma. Kinatujulisha vilevile ya kwamba Bwana Yesu atafunuliwa siku nyingine kwa watu wa dunia, na ya kuwa atakuja katika utukufu kuazibu adui zake na kusimamisha ufalme wake duniani. Kinatuambia juu ya hukumu ya mwisho ya waovu na juu ya utukufu wa mbi ngu.

Katikati ya kitabu cha tano na kitabu cha mwisho cha Agano Jipya, kuna vitabu vingine 21. Vitabu hivi vinaitwa barua. Ni barua zilizoandikwa kwa kufundisha Wakristo. Vitabu vile vili - andikwa na mitume, zaidi na Paulo, na viliandikwa kwa sababu mbalimbali. Nyingine, kama barua kwa Waroma, ziliandikwa kwa kufundisha Wakristo juu ya wokovu na uzima katika Kristo. Nyingine, kama 1 Wakorinto, ziliandikwa kwa kuonya Wakristo waliokuwa wakitenda mabaya, na kuwaonyesha namna gani iliwapasa kutenda. Nyingine, kama Wakolosayi, ziliandikwa kuonya Wakristo juu ya watu waliokuwa wakifundisha maneno mabaya. Sharti usome barua hizi zote moja moja, polepole, hata uone kwa nini kila barua iliandikwa, na halafu inapasa kuzisoma tena mara ya pili, ukikumbuka kwa sababu gani kila barua iliandikwa. Kwa njia hii tu utaweza kufahamu mafundisho ya barua hizi kabisa kabisa.

Ni neno kubwa sana kwa Wakristo kufahamu barua hizi vizuri. Zinafundisha juu ya maneno mengi ambayo inatupasa kujua. Zinaonyesha namna gani tunaweza kuokolewa, na kwa nini tunahitaji wokovu. Zinatupasha juu ya uzuri na mapendo ya Mungu wetu. Zinatupasha juu ya Roho Mtakatifu na juu ya mi - shangao anayotaka kufanya ndani ya maisha yetu. Vilevile zinatuonya juu ya walimu wa uwongo. Hili ndilo neno kubwa kwa wakati wa sasa, wakati watu wingi wanapoonekana katika Afrique, na katika inchi nyingine vilevile, wakifundisha wongo.

Walimu hawa wa uwongo wanakokota watu wingi kuwasikiliza na kupokea maneno wanayosema, kwa sababu kuna watu wachache tu wanaojua na kufahamu barua za Agano Jipya kabisa kabisa. Wakristo wakijifunza barua hizi vizuri, wa limu wa uwo - ngo hawana njia kuwadanganya. Ni kwa sababu ya neno hili, kitabu hiki kiliandikwa, kwa kukusaidia kufahamu maneno waandishi wa barua hizi za Agano Jipya waliyotaka kusema.

Biography of 

Mr. A.E. Horton translated the Bible into the Luvale language of Africa, and explained the meaning of Scripture for many years. In this book 21 Letters for the 21st Century, he gives a short summary of each New Testament epistle. This will prepare you to read these letters again more carefully, and help you to understand more difficult books written on theses epistles. More…


Other Titles by Albert E. Horton


Bible

  Spiritual Growth

  Bible Study

  Doctrinal

   Youth Books

    Devotional Books

     Missionary Books

      Other Books

       Hymn Books